Loading...

Hii hapa 'draw' kamili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya [UEFA]


Klabu ya Tottenham itakabiliana na mabingwa watetezi wa kombe la vilabu bingwa Ulaya Real Madrid katika awamu ya kimakundi ya kombe hilo.

Spurs wamewekwa katika kundi H pamoja na Real Madrid, Mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund na Apoel ya Urusi.

Droo hiyo inamuweka winga wa Real Madrid Gareth Bale na klabu yake ya zamani Tottenham.

Bale alihamia Real Madrid kutoka Tottenham 2013.

Mabingwa wa Uskochi Celtic wanakabiliwa na kibarua kigumu katika kundi moja na Bayern Munich , PSG na Anderlecht.

Mabingwa wa Uingereza Chelsea wamewekwa katika kundi moja na Atletico Madrid, Roma na Qarabag katika kundi Cha , huku mabingwa wa kombe la Yuropa Manchester United wakikabiliana na Benfica, Basle na CSKA Moscow katika kundi A.

Manchester City watamenyana dhidi ya Shakhtar Donetsk, Napoli na Feyenoord katika kundi F huku liverpool ikikabiliana na Spartak Moscow, Sevilla na Maribor katika kundi E.

Hivi ndivyo ilivyo:

Group A:
  • Benfica
  • Manchester United
  • Basel
  • CSKA Moscow
Group B:
  • Bayern Munich
  • Paris St-Germain
  • Anderlecht
  • Celtic
Group C:
  • Chelsea
  • Atletico Madrid
  • Roma
  • Qarabag
Group D:
  • Juventus
  • Barcelona
  • Olympiakos
  • Sporting
Group E:
  • Spartak Moscow
  • Sevilla
  • Liverpool
  • Maribor
Group F:
  • Shakhtar Donetsk
  • Manchester City
  • Napoli
  • Feyenoord
Group G:
  • Monaco
  • Porto
  • Besiktas
  • RB Leipzig
Group H:
  • Real Madrid
  • Borussia Dortmund
  • Tottenham
  • Apoel
Hii hapa 'draw' kamili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya [UEFA] Hii hapa 'draw' kamili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya [UEFA] Reviewed by Zero Degree on 8/25/2017 12:04:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.