Kituo cha kuhesabia kura cha upinzani nchini Kenya chavamiwa
Hali ilivyokuwa ndani ya ofisi hizo |
Nyaya zikiwa zimetupwa |
Msemaji wa NASA ameeleza kuwa wanaume waliokuwa wamefunika nyuso zao walivamia ofisi hiyo wakafanya uharibifu na kubeba kompyuta, simu za mkononi na vitabu.
Kwa upande wake, serikali ya nchi hiyo imesisitiza kuwa hakuna uvamizi uliofanyika, . Mgombea wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa atakubali tu kushindwa ikiwa uchaguzi utakuwa wa haki.
Aidha watu 20 wamekamatwa wakishukiwa kuhusika na uvamizi huo wakiwa na silaha aina ya rifles na bastola.
Hivi karibuni, Rais wa Uhuru Kenyatta alikaririwa akisema ataheshimu matokeo ya uchaguzi huo wa siku ya Jumanne licha ya kila mmoja kusisitiza kuwa ataibuka mshindi.
Uchaguzi wa Kenya mara nyingi umekua ukikumbwa na ghasia. Zaidi ya watu 1000 waliuawa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Nyaya zikiwa zimeharibiwa |
Kituo cha kuhesabia kura cha upinzani nchini Kenya chavamiwa
Reviewed by Zero Degree
on
8/05/2017 08:12:00 PM
Rating: