Loading...

Lissu ameachiwa huru kwa dhamana

Mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu 
Mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu ameachiwa huru kwa dhamana.

Akizungumza mara baada yakutoka nje ya kituo Kikuu cha Polisi wakili wake Peter Kibatala amesema Lissu ameachiwa kwa dhamana na atatakiwa kurudi tena Jumatatu. 

Baada ya kutoka nje ya kituo cha polisi Lissu hakutakiwa kuzungumza chochote kutokana na masharti ya dhamana badala yake aliingia moja kwa moja kwenye gari ya wakili wake.

Kibatala amesema Lissu anatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi pamoja na kumkashfu Rais.
Lissu ameachiwa huru kwa dhamana Lissu ameachiwa huru kwa dhamana Reviewed by Zero Degree on 8/24/2017 07:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.