Loading...

Bakwata yatangaza Sikukuu ya Idd Tarehe 1 Septemba, 2017

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Bin Zubeir 
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeir amesema Septemba Mosi itakuwa ni Sikukuu ya Eid El-Adhaa baada ya mwezi Dhil-Hijjah (mfungo tatu) kuandama Magharibi, Agosti 22 mwaka huu.

Mufti ameeleza hayo katika mkutano na wanahabari leo Alhamisi Agosti 24 katika hotuba yake iliyosomwa na msemaji wake Sheikh Khamis Mataka.

Mkutano huo umefanyika katika makao makuu ya Baraza la Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), Kinondoni ambapo Mufti Zubeir amesema baada ya mwezi huo kuandama na Agosti 23 mwaka huu ilikuwa ni sawa na Mwezi Mosi Mfungo Tatu (Dhul-Hijjah)1438 Hijiriyyah.

"Napenda kuutangazia umma kuwa nimethibitisha mwandamo wa mwezi na kwamba siku ya Agosti 31 ni siku ya kufunga Sunna ya Araf.Wakati Septemba Mosi ni sikukuu," amesema Mufti Zubeir kupitia msemaji wake huyo. 

Amesema maadhimisho ya sikukuu hiyo kitaifa yatafanyika Dar es Salaam na swala itafanyika katika uwanja wa Garden, nyumba ya Msikiti wa Taqwa uliopo Ilala Bungoni huku Baraza la Eid likifanyikia katika eneo hilo pia.

Kupitia sikukuu hiyo, Mufti Zubeir amewahimiza Waislamu kuzidisha ibada na kufanya kheri katika siku 10 tukufu za mfungo tatu na kuichukua vyema falsafa ya Hijja katika kudumisha umoja ja mshikamano miongoni mwao.

"Waislamu watumie kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wa Kiislamu kutafakari na kumchamungu na kuimarisha maadili mema ndani ya jamii itakayokuwa bora na ya kupendana," amesema Mufti Zubeir.
Bakwata yatangaza Sikukuu ya Idd Tarehe 1 Septemba, 2017 Bakwata yatangaza Sikukuu ya Idd Tarehe 1 Septemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 8/24/2017 04:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.