Loading...

Liverpool wamekubali kulipa paundi milioni 35 kumnasa Alex Oxlade-Chamberlain


Liverpool wamekubali kulipa kiasi cha paundi milioni 35 kwa ajili ya kumnasa kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza na Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain.

Nyota huyo mwenye miaka 24, ambaye alikataa kujiunga na Chelsea jana Jumanne baada ya klabu hizo mbili kufikia makubaliano, atajiunga na klabu ya Liverpool kwa mkataba wa miaka mitano ambao utamwingizia paundi 120,000 kwa wiki.

Oxlade-Chamberlain, ambaye yuko kwenye mwaka wake wa mwisho kumalizia mkataba na klabu ya Arsenal, alikataa kubaki
 Emirates kwa kugoma kusaini mkataba mpya ambao ungemwingizia paundi 180,000 kwa wiki.

Hata hivyo, ameanzishwa kwenye kikosi cha kwanza katika mechi zote nne ambazo Arsenal wameshacheza hadi hivi sasa katika msimu huu.

Oxlade-Chamberlain ameichezea Arsenal michezo 198 tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Southampton mwezi Agosti mwaka 2011, akiifungia Arsenal jumla ya magoli 20.

Ada hiyo ingeweza kuwa ni moja wapo ya ada za kihistoria kwa klabu ya Liverpool, lakini tayari wamekwisha kubali kulipa kiasi cha paundi milioni 48 kumnasa nyota wa RB Leipzig's, Naby Keita katika majira ya joto mwakani.

Hadi hivi sasa katika majira haya ya joto, Liverpool wamefanikiwa kumsajili Mohamed Salah kutokea Roma kwa paundi milioni 34, beki wa pembeni, Andrew Robertson kutokea Hull City kwa paundi milioni 8 na mshambuliaji Dominic Solanke baada ya mkataba wake na Chelsea kumalizika.

Liverpool pia wamekuwa mstari wa mbele katika kusaka saini ya winga wa Monaco, Thomas Lemar anayekadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 75 pamoja na beki wa kati wa klabu ya Southampton, Virgil van Dijk, wakati huo huo mshambuliaji wao kutoka Brazil, Philippe Coutinho akibakia kuwa chaguo la kwanza kwa Barcelona.

Pia kuna uwezekano mkubwa kwa mshambuliaji wa Liverpool mwenye asili ya kibeligiji, 
Divock Origi kuondoka Anfield na kujiunga na Wolfsburg ya Ujerumani kwa mkopo  kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya alhamisi.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 ni mmoja wa wachezaji pendwa wa meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp, lakini kwa Oxlade-Chamberlain kuwasili akitokea Arsenal imaana nafasi yake dimbani itakuwa ni ya mashaka kwa msimu huu.

Origi anapenda kuwa mchezaji wa kudumu kwenye kikosi cha kwanza katika kipindi chote kilichosalia kuelekea  fainali za kombe la dunia mwaka 2018 na Liverpool pia watapendelea kuona nyota huyo akiendelea kujiimalisha kimchezo, hivyo anatarajiwa kuondoka Anfield kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Liverpool wamekubali kulipa paundi milioni 35 kumnasa Alex Oxlade-Chamberlain Liverpool wamekubali kulipa paundi milioni 35 kumnasa Alex Oxlade-Chamberlain Reviewed by Zero Degree on 8/30/2017 11:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.