Loading...

Mike Pence akanusha kujiandaa kuwania urais mwaka 2020


Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence amekana vikali madai ya ripoti zinazodai kuwa anajiandaa na kuwania urais wa Marekani mwaka 2020.

Gazeti la The New York Times lilisema kuwa kampeni za pembeni zimepangwa kufuatia madai yanayoeleza kuwa Donald Trump hatawania tena.

Likinukuu vyanzo tofuati tofauti, ripoti ya gazeti hilo ilisema kuwa bwana Pence anaweza kuwania Urais ikiwa Donald Trump hatawania tena.




Lakini kwa upande wake, Mike Pence amesema kuwa ripoti hiyo ni jaribio la kuvuruga uongozi.

Mshauri wa cheo cha juu katika ikulu ya White House Kellyanne Conway pia aliitupilia mbali ripoti hiyo.

"Ni ukweli kuwa makamu wa rais anajiandaa kwa mwaka wa 2020, kuchaguliwa tena kama makamu wa rais", aliliambia shirika la ABC.

Msemaji wa gazeti la New York Times alitetea ripoti hiyo akisema wana imani na taarifa zao na wataiachia ripoti hiyo kuijieleza yenyewe.
Mike Pence akanusha kujiandaa kuwania urais mwaka 2020 Mike Pence akanusha kujiandaa kuwania urais mwaka 2020 Reviewed by Zero Degree on 8/07/2017 11:19:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.