Loading...

Video: Arsenal walivyojibebea Kombe la Ngao ya Hisani kwenye uwanja wa Wembley


Klabu ya Arsenal imefanikiwa kuchukua kombe la Ngao ya Hisani kwa mwaka 2017 baada ya kuifunga Chelsea 4-1 kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 mchezo ulipigwa katika uwanja wa taifa wa Uingereza, Wembley jioni ya jana.

Mpaka dakika 45 za mchezo wa kwanza kumalizika hakuna timu yoyote iliyoweza kuchungulia nyavu za mwenzake japokuwa wachezaji wa pande zote mbili walionekana kujitutumua kupata bao la ushindi, lakini ilipofikia dakika 46 ya kipindi cha pili mchezaji Victor Moses aliweza kupachika bao la kwanza na kuifanya Chelsea kuwa mbele kwa goli 1.

Mbali na goli hilo, timu ya Chelsea ilionekana kumiliki mpira kwa muda mrefu na mpaka ilipofikia dakika 81 bao hilo liliweza kusawazishwa kwa mkwaju wa adhabu uliyopigwa na mchezaji Sead Kolašinac kupelekea kuwa sare ya mabao na mpaka kipenga cha mwisho kilipopulizwa hakuna bao lingine lililofungwa toka katika timu hizo na kusababisha kwenda mikwaju ya penati ili aweze kupatikana bingwa wa kombe la Ngao ya Hisani kwa mwaka 2017.

Kwa upande mwingine, timu ya Arsenal iliweza kujishindia penati 4 zilizopigwa kiufundi na wachezaji Theo Walcot, Nacho Monreal, Alex Oxlade-Chamberlain pamoja na Olivier Giroud huku upande wa Chelsea wakipata mkwaju mmoja uliyopigwa na Gary Cahill.


Video: Arsenal walivyojibebea Kombe la Ngao ya Hisani kwenye uwanja wa Wembley Video: Arsenal walivyojibebea Kombe la Ngao ya Hisani kwenye uwanja wa Wembley Reviewed by Zero Degree on 8/07/2017 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.