Loading...

Mtoto apotea katika mazingira ya kutatanisha


MTOTO aitwaye Kaira Kibela (2), mkazi wa kitongoji cha Kaloleni Mlandizi, Wilaya ya Kibaha Vijijini mkoani Pwani, amepotea katika mazingira ya kutatanisha na kuibua hofu kubwa.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kaloleni, Kilindo Ally, aliliambia Gazeti la Nipashe mwishoni mwa wiki kuwa, mtoto huyo (pichani) alipotea Jumapili iliyopita, majira ya saa 3:00 asubuhi wakati akicheza na wenzake. 

Alisema hadi sasa wanaendelea kumtafuta na tayari wameshatoa taarifa katika kituo cha polisi Mlandizi.

Ally aliwataka wananchi wasaidie kupatikana mtoto huyo kwa kutoa taarifa pindi watakapomuona, kupitia polisi au kupiga simu namba 0763211081.
Mtoto apotea katika mazingira ya kutatanisha Mtoto apotea katika mazingira ya kutatanisha Reviewed by Zero Degree on 8/05/2017 08:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.