Loading...

So Campbell atua nchini kwa mwaliko wa SportPesa


Beki kisiki wa zamani wa Arsenal, So Campbell tayari ametua nchini kwa ajili ya ziara ambayo ni mwaliko wa SportPesa Tanzania.

Campbell ametua na kupokelewa na wenyeji wake SportPesa na baadaye mashabiki wa Arsenal ambao walijitokeza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kumpokea.


Mashabiki wa Arsenal waliokuwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kumpokea, walipata nafasi ya kupiga naye picha pamoja.

Baada ya kuwaona mashabiki hao, Campbell ambaye yuko nchini kwa mwaliko wa SportPesa, aliwafuata na kujumuika nao wakipiga picha pamoja kwa furaha.


Mara tu baada ya kutua nchini, beki kisiki wa zamani wa Arsenal, So Campbell tayari amekwenda moja kwa moja kutembelea timu ya walemavu ya Muungano.

Campbell ametua nchini kwa ajili ya ziara ambayo ni mwaliko wa SportPesa Tanzania. Alipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa timu hiyo ambao walimwelezea namna ilivyoanzishwa na wanavyoendelea.

Campbell ni katiya mabeki visiki waliowahi kutokea nchini England. Pia ni kati ya mabeki waliocheza kwa mafanikio makubwa katika kikosi cha Arsenal chini ya Kocha Arsene Wenger.
So Campbell atua nchini kwa mwaliko wa SportPesa So Campbell atua nchini kwa mwaliko wa SportPesa Reviewed by Zero Degree on 8/05/2017 08:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.