Loading...

Ushauri wa Frank Lampard kwa Klabu ya Chelsea


Aliyekuwa kiungo wa Chelsea, Frank Lampard ameipa ushauri wa bure klabu yake ya zamani kuhusiana na usajili.

Lampard anaamini kwamba, Antonio Conte anatakiwa kusajili kiungo mwingine kwa ajili ya kuongeza nguvu katikati kufuatia kuondoka kwa Nemanja Matic.

Chelsea wamekwisha msajili Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco lakini Lampard anasema kuwa, hiyo haitoshi.

Lampard anaamini 'The Blues' bado wanatakiwa kupata nyota wapya zaidi kwa ajili ya mahitaji ya ziada yanayoweza kujitokeza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lampard aliiambia 'BT Sport' kuwa “Nafikiri wanahitaji mchezaji mwingine katika kiungo. Wanamsubiria Tiemoue Bakayoko kuwa katika hali nzuri arejee dimbani.

“Ni kazi kubwa sana kwa Cesc Fabregas kucheza dhidi ya klabu nyingine kubwa katika michezo yenye upinzani mkubwa kuweza kuhimili mikiki na kuweza kuleta madhara kwenye mchezo.

“Labda hiyo itamsaidia Cesc Fabregas kwenda mbele zaidi kama mshambuliaji na hapo ndipo watakapohitaji atakayefanya kazi ya kuzuia upenyo."
Ushauri wa Frank Lampard kwa Klabu ya Chelsea Ushauri wa Frank Lampard kwa Klabu ya Chelsea Reviewed by Zero Degree on 8/07/2017 02:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.