Loading...

Watu 3 wamefariki dunia katika ajali mbili tofauti zilizotokea Singida


Watu watatu wamekufa katika ajili mbili tofauti wilayani Manyoni ,ikiwemo ya mbunge wa Manyoni mashariki kumgonga mwanafunzi wa darasa la kwanza na kufariki papo hapo ,na ajali nyingine gari aina ya Hiace kuligonga lori kwa nyuma na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo.

Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo kamanda wa polisi mkoani Singida ACP Debora Magiligimba amesema matukio hayo yametokea tarehe kumi mwenzi huu na amemtaja mbunge wa Manyoni mashariki Bwana Daniel Mtuka, aliyekuwa akiendesha gari lenye usajili wa namba T.238 DGU aina ya Prado alimgonga mwanafunzi Salome Paschal wa shule ya msingi Sukamahela aliyekuwa akijaribu kuvuka barabara.

Katika ajali nyingine kamanda Magiligimba amesema gari aina ya toyota hiace iligonga lori kwa nyuma lenye usajili wa namba T.407 DES na tela T.809 CAS aina ya DAF na kusababisha kifo cha dereva raia wa Kongo ambaye hakufahamika jina na afisa elimu sekondari wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bwana Alfred Katega.

Akiongea kwa simu mganga mkuu wa wilaya ya Manyoni Daktari Nelson Bukuru amethibitisha kupokea maiti mbili za ajali ya gari aina ya hiace kulingonga lori ambazo zimepata majeraha kichani na alipotakiwa kueleza ajali ya mbunge kumgonga mwanafunzi simu yake ilikatika na haikupatikana ,ITV haikuishia hapo ilimtafuta mbunge na simu yake ilipokelewa na mtu mwingine na kusema kuwa yupo kwenye kikao.

Ajali zote hizo mbili ambazo zimesababisha vifo vya watu watatu wilayani Manyoni kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Singida amesema zimesababishwa na uzembe wa madereva wa gari aina ya Hiace na Prado.
Watu 3 wamefariki dunia katika ajali mbili tofauti zilizotokea Singida Watu 3 wamefariki dunia katika ajali mbili tofauti zilizotokea Singida Reviewed by Zero Degree on 8/12/2017 10:01:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.