Loading...

Antonio Conte afunguka kuhusu kadi nyekundu ya David Luiz


David Luiz alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya mchezaji wa Arsenal, Saed Kolasinac.

Antonio Conte ameelezea rekodi ya klabu kuandamwa na kadi nyekundu hivi karibuni kama "ajabu" na kupendekeza kwamba timu yake inahitaji "kuwa na bahati kubwa" kwa waamuzi wa mchezo.

Conte pia hakutaka kukaliliwa kuwa alichukulia kitendo cha Luiz kupewa kadi nyekundu kama haki kwa alichomfanyia Sead Kolasinac.




Kuhusu David Luiz, unajua vizuri kabisa kwamba sipendi kutoa maoni yoyote kuhusu mwamuzi, alisema Conte na kuongeza: Sikufanya hivyo miaka iliyopita, au sasa. Unatakiwa kuona kilichotokea kabla ya maamuzi.

Tunaheshima kubwa kwa waamuzi, lakini ni ajabu kumaliza mchezo wa tatu mfululizo dhidi ya Arsenal tukiwa na wachezaji 10 uwanjani.

“Tunafanya kazi kujiimirisha katika suala la mbinu za kimchezo na kuiweka miili sawa kwa mchezo. Mwisho wa siku, tutajaribu kuwa makini wakati ujao. Natumaini, pia, tutakuwa na bahati nzuri na maamuzi yanayotolewa na waamuzi mchezoni. Kwetu sisi, na pia kwa wapinzani wetu. Wakati mwingine wapinzani ndio wanaostahili kupewa kadi nyekundu lakini wanaendelea uwanjani wakiwa watu 11. Hivyo unajikuta unatakiwa kuwa mwenye bahati sana wakati ujao.”
Antonio Conte afunguka kuhusu kadi nyekundu ya David Luiz Antonio Conte afunguka kuhusu kadi nyekundu ya David Luiz Reviewed by Zero Degree on 9/18/2017 09:02:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.