Loading...

PSG wahofia kuishiwa jezi za Neymar


Kwa kukisia Paris Saint-Germain wanaweza kuishiwa Jezi za Neymar baada ya kufikia rekodi kubwa ya mauzo.

Kwa mujibu wa taarifa ya 'DailyMail', klabu hiyo ya Ufaransa ina oda ya jezi zaidi ya zile zilizouzwa mwezi uliopita ikiwa tayari ni jezi zaidi ya laki 120 za Neymar zimekwisha uzwa zenye thamani ya paundi milioni 7.8. 

Taarifa ya 'DailyMail' inadai kwamba, Duka la Klabu tayari limeona kuna ongezeko la asilimia 75% kwenye mauzo hadi muda huu ukilinganisha na yale ya msimu uliopita, ikidaiwa kwamba mauzo hayo yamechangiwa na kuwasili kwa raia huyo wa brazili.

Lakini kwa ongezeko hilo, PSG wamebakiwa na kiasi cha jezi za Neymar ambazo zinaweza kutosheleza hadi mwezi Novemba tu, hivyo wanahofia kuishiwa kabla ya muda uliotegemewa.

Mbrazili huyo amehamishia maisha yake ya soka nchini Ufaransa kama vile bata anayeogelea majini kufuatia kuweka rekodi kubwa kwenye usajili kwa kusajiliwa kwa kiasi cha paundi milioni 198 akitokea barcelona kwenye majira ya joto, ambapo hadi hivi sasa ndiye mchezaji ghali zaidi duniani na tayari anaonekana kuwa mchezaji anayependwa na mashabiki wengi ndani ya klabu hiyo.




Neymar ameonyesha uwezo mkubwa tayari tangu ajiunge na klabu hiyo na amefanikiwa kuifungia magoli matano pia kutoa 'assist' za kutosha kwenye michuano yote.

PSG watapendelea kumuona nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 akiendelea kuwa kwenye kiwango kizuri wakati watakapokuwa kwenye jaribio lao gumu la kwanza kwenye mashindano ya kuwania taji la Ligue 1 dhidi ya Lyon siku ya Jumapili jioni.
PSG wahofia kuishiwa jezi za Neymar PSG wahofia kuishiwa jezi za Neymar Reviewed by Zero Degree on 9/18/2017 03:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.