Loading...

Hii hapa rekodi mpya ya Jurgen Klopp Uingereza


Klabu ya Liverpool inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imeonekana kuwa ndiyo timu yenye kupata matokeo bora zaidi dhidi ya zile zilizopo ndani ya sita bora ya ligi Kuu ya Uingerza (EPL) tangu ianze kunolewa na Meneja, Jurgen Klopp.

Liverpool imekuwa yenye mafanikio makubwa miongoni mwa timu kubwa za Uingereza tangu, Jurgen Klopp kurithi mikoba ya Brendan Rodgers katika dimba la Anfield mwezi Octoba mwaka 2015.

Chini ya Klopp, Liverpool imeshinda michezo yake ya ligi kwa asilimia 47 huku ikivuna alama 33 katika michezo yake 18 iliyokutana na miamba ya soka ya Uingereza Tottenham, Manchester City, Arsenal huku ikishindwa kufanya hivyo mbele ya Manchester United mwezi Januari mwaka uliopita.

Kwa ushindi wao wa michezo tisa ikijumuishwa mitatu dhidi ya Manchester City, mitatu na Arsenal miwili mbele ya Chelsea na mmoja dhidi ya Tottenham.

Huku Arsenal ikipokea kipigo cha mabao 4-0 chini ya Meneja Klopp katika mchezo uliyopigwa kwenye dimba la Anfield mwezi uliopita.

Swali ni, Je Liverpool itaendeleza rekodi yake mbele ya Manchester City katika dimba la Etihad siku ya Jumamosi?

Hii hapa rekodi mpya ya Jurgen Klopp Uingereza Hii hapa rekodi mpya ya Jurgen Klopp Uingereza Reviewed by Zero Degree on 9/08/2017 07:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.