Loading...

Wakimbizi wa Burundi waanza kurejea kwao

Hadi  kufikia Desemba, wakimbizi zaidi ya 10,000 wanatarajiwa kuwa wamerejea Burundi
Wakimbizi 302 wa Burundi ambao wamekuwa wakiishi katika nchi jirani ya Tanzania wamerejea nchini mwao hivi leo kutoka kambi ya Nduta wilaya ya Kibondo mkooani Kigoma, mashariki mwa Tanzania.

Kurejea kwa wakimbizi hao ni sehemu ya kwanza ya kampeni ya kuwahamisha wakimbizi takriban elfu 12 kufikia mwezi Desemba.

Wakimbizi hao wamesafirishwa kwa mabasi hadi nchini Burundi.

Mmoja wa wakimbizi hao kwa jina Madelena aliiambia BBC: "Kambini Nduta tulikua na maisha magumu. Chakula tulikua tukipewa kwa uchache. Tukienda kutafuta kuni baadhi walikuwa wakikutana na majambazi na kuvamiwa. Nimeona bora nirudi nyumbani."

Mwingine kwa jina Angelina amesema: "Mimi naelekea nyumbani kwetu nimerudi na mume wangu na watoto watatu. Nitafika ninalima. Nina taarifa kuwa shamba langu lipo. Naelekea mkoani Chibitoke."

Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la wakimbi la Umoja wa Mataifa UNHCR iliyotolewa mwezi Juni, kufikia wakati huo, kulikuwa na wakimbizi 241,000 kutoka Burundi waliopatiwa makazi nchini Tanzania.

Katika idadi hii kubwa ya watu wanaokimbia nchi yao, UNHCR inasema asilimia 60 ni watoto.

Na ndani ya kipindi cha miezi mitano tu ya mwaka huu wa 2017, wakimbizi 44,487 wamekimbia Burundi na kuingia Tanzania.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Serikali ya Tanzania ililipatia shirika la wakimbizi duniani UNHCR siku saba kuanza kuwarudisha wakimbizi wa Burundi ambao wanataka kurudi kwao kwa hiari, ama sivyo serikali yenyewe ifanye zoezi hilo yenyewe.

Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Mwigulu Nchemba alitoa agizo hilo alipokuwa katika ziara ya kikazi katika kambi ya Nduta Magharibi mwa Tanzania ambayo ni moja ya kambi zinazohifadhi wakimbizi wengi wa Burundi.

Baada ya makataa hayo kumalizika, maafisa wa serikali walikutana na maafisa wa UNHCR.
Wakimbizi wa Burundi waanza kurejea kwao Wakimbizi wa Burundi waanza kurejea kwao Reviewed by Zero Degree on 9/08/2017 07:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.