Jibu la Diego Costa baada ya kuulizwa kama ana chuki dhidi ya Conte
Chelsea walitangaza kufikia makubaliano na klabu ya Atletico Madrid jana Alhamisi na kukubali kumuachia Costa arejee Uhispania kwa zaidi ya paundi milioni 50.
Conte alimuacha Diego Costa kando akidai hayumo kwenye mipango yake kikosini licha ya nyota huyo kufunga magoli 20 katika michezo 35 na kuisaidia Chelsea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita.
Conte alimuacha Diego Costa kando akidai hayumo kwenye mipango yake kikosini licha ya nyota huyo kufunga magoli 20 katika michezo 35 na kuisaidia Chelsea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita.
Costa alikataa kurejea kwenye kambi ya mazoezi ya Chelsea katika majira ya joto, badala yake akabakia Brazil akitumaini kwamba Atletico wataingilia kati suala hilo na kumrudisha Madrid.
Akiwa Sao Paulo, aliulizwa kama anamchukia Antonio Conte kwa kitendo hicho alichomfanyia, Costa alijibu: "Hakuna lolote kabisa, wala sijachukizwa na sina kinyongo na mtu yeyote. Kila kitu kipo sawa."
Alipoulizwa kama ana ujumbe wowote kwa mashabiki, aliongeze: "Kila mtu anajua ni kiasi gani ninawapenda mashabiki."
Atletico walishindwa kulikazia mkazo suala la usajili wake kabla dirisha la usajili halijafungwa, ikiwa pia ni hofu kumshuhudia Costa akiwa benchi bila kuichezea timu hadi adhabu yao itakapokuwa imeisha mwezi Januari.
Costa hajacheza kwa muda wa siku 98 tangu aonekane kwa mara mwisho kwenye mechi ya Spain na Macedonia kwenye michuano ya kufuzu kushiriki kombe la dunia 2018.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alifunga magoli 20 kwenye mechi 35 za Ligi Kuu ya Uingereza ambapo Chelsea ndio waliobeba taji hilo, lakini aliachwa katika mazingira ya kutatanisha na kocha wake.
Costa aliitumikia Atletico kwa miaka minne kabla hajajiunga na Chelsea mwezi Julai mwaka 2014 kwa paundi milioni 32.
Alifanikiwa kufunga magoli 59 ndani ya michezo 120 akiwa na Chelsea, ambapo katika kipindi hicho Chelsea imefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu mara mbili.
Costa aliitumikia Atletico kwa miaka minne kabla hajajiunga na Chelsea mwezi Julai mwaka 2014 kwa paundi milioni 32.
Alifanikiwa kufunga magoli 59 ndani ya michezo 120 akiwa na Chelsea, ambapo katika kipindi hicho Chelsea imefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu mara mbili.
Jibu la Diego Costa baada ya kuulizwa kama ana chuki dhidi ya Conte
Reviewed by Zero Degree
on
9/22/2017 08:17:00 PM
Rating: