Loading...

Kauli ya Waziri Mkuu juu ya waliomshambulia Mhe. Lissu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, jana Septemba 15, 2017 alieelezea juu ya kusikitishwa kwake na tukio la kinyama la kushambuliwa kwa kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu na watu wasiojulikana.


“Kufuatia tukio la kushambuliwa kwa Mbunge mweznetu, Tundu Lissu, naungana na Rais John Pombe Magufuli, makamu wa rais, spika, wabunge na Watanzania wote kumpa pole kwa majeraha na maumivu na majeraha makubwa aliyoyapata, tunamuombea apone haraka ili aweze kurejea kuungana na familia yake na sisi bungeni.


“Pia natoa pole kwa Meja Jenerali Mstaafu, Vincet Mritaba kwa kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Lugalo.

“Nasisitiza kwamba, serikali inawasaka na itawatia nguvuni wote wale wote waliohusika na mashambulio hayo,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Kauli ya Waziri Mkuu juu ya waliomshambulia Mhe. Lissu Kauli ya Waziri Mkuu juu ya waliomshambulia Mhe. Lissu Reviewed by Zero Degree on 9/16/2017 08:52:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.