Loading...

Afikishwa mahakamani kwa kosa la kufunga ndoa na mwanaume mwenzake mkoani Mtwara


Mkazi wa wilaya ya Mtwara, Sharifu Issah maarufu kama Zamda Salumu amemfikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya vitendo vya utovu wa kimaadili kwa kujifanya mwanamke na kumshawishi mwanaume mwenzake kufunga nae ndoa na kuishi pamoja kama mke na mume isivyo halali.

Akisoma kesi hiyo hakimu mkuu mkazi Richard Kabate na kusomewa shitaka na wakili wa serikali George Kaubi Makasi amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 157 cha kanuni ya adhabu sura no 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Amesema tarehe tofauti mshtakiwa kati ya mwezi wa tatu mwaka 2017 na mwezi wa sita 2017 katika vijiji vya Mkahala na Mpanyani halmashauri ya Nanyamba mkoa wa Mtwara kwa makusudi katika jamii alijifanya mwanamke na matokeo yake kumshawishi Mustapha Saidi Nurdini kwa kumtongoza na kufunga nae ndoa isiyo halali.

Hata hivyo hakimu Kabete amesema kitendo hicho kinatoa tafsiri ya ukiukwaji mkubwa wa maadili kwa watu wa jinsia moja ya kiume kuishi kinyumba.

Hata hivyo mshtakiwa aliposomewa shtaka hilo na wakili wa serikali George Makasi amekana shitaka hilo na upelelezi wa kesi hiyo unaendelea.

Mshtakiwa amerudishwa mahabusu , na kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo tarehe 28-09-2017, dhamana iko wazi baada ya mwezi mmoja.

Source: ITV
Afikishwa mahakamani kwa kosa la kufunga ndoa na mwanaume mwenzake mkoani Mtwara Afikishwa mahakamani kwa kosa la kufunga ndoa na mwanaume mwenzake mkoani Mtwara Reviewed by Zero Degree on 9/16/2017 09:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.