Loading...

Spika Ndugai awataka wabunge kuchukua tahadhari juu ya usalama wao


Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amewataka Waheshimiwa Wabunge kuchukua tahadhari juu ya usalama wao mahali popote wanapokuwa ili kujiepusha na matukio ya kihalifu yanayotokea hapa Nchini.

Spika Ndugai ametoa tahadhari hiyo jana Bungeni Mjini Dodoma baada ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Kasim Majaliwa Majaliwa kutoa hoja ya kuahirisha Mkutano wa Nane wa Bunge.

“Tuchukue hatua katika maisha yetu, kama mnavyosikia matukio ni mengi katika Nchi yetu, usalama unanza na wewe kwanza halafu vyombo vya ulinzi vinavyotulinda vinasaidia tu kidogo, tutazame nyendo zetu,” alisema.

Aidha, Mheshimiwa Ndugai amewaomba Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki Mheshimiwa Tundu Lissu pamoja na wale wanaomuuguza wakiwemo waheshimiwa Wabunge.

Vilevile Meshimiwa Spika amewapangia Kamati Waheshimiwa Wabunge wapya wanane(8) wa Chama cha Wananchi (CUF) walioapishwa katika Mkutano huu wa Nane wa Bunge.

Wajumbe hao na Kamati zao ni Mheshimiwa Shamsia Mtamba (Kamati ya Viwanda, Biashara na mazingira), Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmed (Kamati ya Miundombinu),

Zainabu Mndolwa Amir (Kamati ya Katiba na Sheria), Mheshimiwa Alfredina kahigi (Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa), Rehema Migila, Sonia Jumaa Magogo na Nuru Bafadhili (Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii) na Mheshimiwa Kiza Hussen Mayeye (Kamati ya Nishati na Madini).

Mapema akiahirisa Bunge Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa pamoja na mambo mengine amezungumzia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 unaridhisha na kwamba Serikali itaongeza jitahada za kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Amesema katika kipindi cha mwezi Julai mpaka Agosti mwaka huu, Serikali imefanikiwa kukusanya Shilingi Tririoni 2.7 ambapo katika ya mapato hayo Mamlaka ya Mapato (TRA) imekusanya Shilingi Tririoni 2.3.
Spika Ndugai awataka wabunge kuchukua tahadhari juu ya usalama wao Spika Ndugai awataka wabunge kuchukua tahadhari juu ya usalama wao Reviewed by Zero Degree on 9/16/2017 09:47:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.