Loading...

Mahakama yamuachia huru Askofu Gwajima


ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na maaskofu wenzake watatu, wameachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao kushindwa kuhifadhi silaha.

Mbali ya Askofu Gwajima, washitakiwa wengine walioachiwa huru jana ni George Mzava, Msaidizi wake, Yekonia Bihagaze (39) na Georgey Milulu ambao walikuwa wakikabiliwa na mashitaka mawili ya kukutwa wakimiliki Bastola aina ya Berretta pamoja na risasi 20 kinyume cha sheria.

Akisoma jukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha alisema kuwa kesi hiyo haijathibitika kwa viwango vinavyotakiwa na kwamba begi lililokuwa na bunduki na risasi virudishwe kwa Askofu Gwajima. Alisema kuwa hakuna uthibitisho kwamba Gwajima alizembea kusalimisha silaha hizo Polisi.

“Hakuna ubishani kwamba Askofu Gwajima alikubali kuripoti katika Ofisi ya Mpelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO) ambapo alifika akiwa na begi lake lenye bunduki na risasi 20.

Na hakuna ushahidi kama mshitakiwa alikaguliwa alipoingia Polisi hadi alipokutana na ZCO na kwamba wakati anahojiwa alipoteza fahamu akiwa na begi lake hadi alipozinduka akiwa Hospitali ya TMJ,” alisema Hakimu Mkeha.

Pia alisema mshitakiwa huyo alikuwa makini nyakati zote akiwa na silaha zake kwani hata alipokuwa kitandani aliilinda. Alisisitiza kuwa ushahidi wa nesi kutoka TMJ ulionesha ni namna gani Polisi walitumia nguvu kupata begi hilo hadi mshitakiwa wa pili alipoamua kumkabidhi mshitakiwa wa pili ili ampatie polisi.

“Ingawa sheria kwa namna yoyote haielezi ni lazima shahidi fulani aje lakini kwa mazingira yaliyokuwepo hospitali ambayo kulikuwa na walinzi hawa wangeweza kuletwa kwa mashahidi wa upande wa mashitaka lakini hawakuletwa na hawakuingizwa kama wazembe katika kesi hii, hii inaongeza shaka kwa upande wa mashitaka,” alisema.

Alisisitiza kuwa mashitaka hayo yana mashaka kwa sababu hakupata sababu za msingi za kutokuamini ushahidi wa nesi aliyeeleza namna tukio lilivyotokea hivyo hapaswi kupingwa hivyo.

Wanadaiwa kuwa Machi 29, 2015 katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A walikutwa wakimiliki Bastola aina ya Berretta yenye namba ya siri CAT 5802 bila ya kuwa na kibali toka kwa mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.

Inadaiwa kuwa washitakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 32 (1) na cha 34 (1)(2) na (3) cha sheria ya Silaha na Milipuko sura ya 223 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010. Pia wanadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio washtakiwa hao pia walikutwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu za Bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya Shotgun.
Mahakama yamuachia huru Askofu Gwajima Mahakama yamuachia huru Askofu Gwajima Reviewed by Zero Degree on 9/16/2017 10:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.