Loading...

Mabasi ya mwendo kasi yagogana Jijini Dar


Abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka (Udart) wamekwama Kimara kutokana na kukosekana huduma kulikosababishwa na ajali iliyotokea Shekilango, Ubungo.

Vituo vya Udart vilivyoko Mbezi Mwisho hadi Ubungo vimefurika abiria baadhi wakiamua kutafuta usafiri mbadala.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Udart, Deus Bugaywa amesema gari moja liligonga lingine kwa nyuma hivyo kusababisha barabara kutopitika.

Bugaywa amesema baada ya mabasi ya Udart yaliyogongana kuondolewa, hivi sasa wanachofanya ni kuhakikisha abiria wote walio vituoni wanapata usafiri.
Mabasi ya mwendo kasi yagogana Jijini Dar Mabasi ya mwendo kasi yagogana Jijini Dar Reviewed by Zero Degree on 9/15/2017 01:22:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.