Loading...

Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari kwa wakazi wa ukanda wa pwani

Picha ya Mtandao
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi katika maeneo ya ukanda wa Pwani.

Kwa mujibu wa taarifa TMA inasema kuanzia leo (Jumamosi) hadi Septemba 5 mwaka huu kutakuwa na upepo mkali unaozidi kasi ya kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0.

Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuwa msukumo wa upepo wa Kusi mashariki unatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda wa Pwani ya Tanzania.

Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari kwa wakazi wa ukanda wa pwani Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari kwa wakazi wa ukanda wa pwani Reviewed by Zero Degree on 9/02/2017 07:51:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.