Loading...

Taifa Stars yaichakaza Botswana goli 2-0


TIMU ya Taifa ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars imeinyuka Timu ya Botswana bao 2-0, mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya FIFA ambao umepigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo, mshambuliaji wa Stars, Simon Msuva anayekipiga Difaa Eljadida ya Morocco ameibeba Tanzania baada kupachika bao zote mbili ambapo bao la kwanza amefunga dakika ya 5 ya kipindi cha kwanza na kurudi tena wavuni kunako dakika ya 61 ya mchezo huo.

Kunako dakika ya 20, Mbwana Samatta alimchomekea Msuva pasi maridadi ambayo alizama nayo moja kwa moja langoni kwa kuachia mkwaju mkali uliomshinda kipa wa Botswana na kuwafanya Watanzania kunyanyua vinywa wakishangilia bao hilo.

Mchezo ulikuwa mzuri na wa kusisimua huku timu zote mbili zikishambuliana kwa zamu licha Stars kuwazidi mbinu Botswana na kuibuka na ushindi huo.
Taifa Stars yaichakaza Botswana goli 2-0 Taifa Stars yaichakaza Botswana goli 2-0 Reviewed by Zero Degree on 9/02/2017 07:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.