Loading...

Mexico: Tetemeko la ardhi laua watu zaidi ya 140

Waokoaji wakijitahidi kuwatoa watu katika vifusi
Tetemeko baya la ardhi limekumba maeneo ya katikati mwa Mexico na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 140.

Tetemeko lenye nguvu ya kipimo cha saba nukta moja limedondosha karibu majengo 30 katika mji mkuu wa Mexico city.

Watu wanaotoa huduma za dharura wakisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea bado wanaendelea kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi.

Maafisa wa serikali nchini wanasema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.

Daniel Lieberson alikuwa katika hotel ya Hilton Mexico City wakati tukio hilo likitokea.

''...Nilikuwa katika ghorofa ya 26. jengo lilikuwa likiyumba mbele na nyuma vioo vyote vilivunjika na tuliogopa kwamba madirisha yatavunjika, lakini haikuwa hivyo. Lakini mashine ya kutengenezea kahawa na vitu vingine vilianguka chini vyote, meza, ilikuwa shida kweli, lilidumu kwa sekunde thelathini tu, lakini ilionekana kama limedumu daima...'' anasema Daniel Lieberson

Kwa upande wake Natasha Pizzey mwandishi wa habari katika mji huo anasema kuna idadi kubwa ya watu waliofukiwa na kifusi baada ya majengo kuporomoka.

Juhudi za uokoaji zikiendelea
''..Tunafahamu kuna watu walionusurika katika majengo ya makazi yaliyoporomoka, hatukuwa na uwezo wa kuwaokoa. Kuna mamia ya wafanyakazi wa kujitolea waliokwenda katika eneo la tukio...'' ameongezea kusema

Aidha pia kumetokea madhara mabaya katika majimbo ya jirani ya Morelos na Puebla.

Mapema mwezi huu tetemeko hilo la ardhi pia lilipita katika eneo la pani ya kusini magharibi mwa Mexico na kusababisha vifo vya watu 90.
Mexico: Tetemeko la ardhi laua watu zaidi ya 140 Mexico: Tetemeko la ardhi laua watu  zaidi ya 140 Reviewed by Zero Degree on 9/20/2017 08:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.