Loading...

Mwenyekiti wa CCM na katibu wake wajiuzulu uongozi


MWENYEKITI wa chama cha mapinduzi (CCM) Tawi la Bugoyi Kata ya Ndembezi mjini Shinyanga Mashaka Said na Katibu wake Samson Chuma, wamejiuzulu nyazifa hizo kwa madai ya kulemewa na majukumu ya kulea familia zao.

Viongozi hao wa CCM walijiuzulu kwa nyakati tofauti, lakini wote wakitoa maelezo ya aina moja kuwa hawawezi kuendelea kukitumikia chama hicho, ikiwa wametingwa na majukumu ya kulea familia zao ,na hakuna sababu zingine zilizowafanya kuachia madaraka hayo.

Akizungumzi suala hilo mwenyekiti Said alisema, ameamua kujiuzulu kutoendelea na madaraka hayo kwani ana majukumu mengine ya kulea familia yake, hivyo hawezi tena kuendelea kukitumikia chama hicho, na kuamua kuachia watu wengine wakifanyie kazi.

Naye Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Chalres Sangula, alikiri kupokea taarifa za kujiuzulu kwa viongozi hao wa Tawi, na kutoa sababu hizo hizo za kulemewa na majukumu ya kifamilia, na kutokujua kiundani nini tatizo hasa ambalo limewasibu kuachia madaraka hayo.
Mwenyekiti wa CCM na katibu wake wajiuzulu uongozi Mwenyekiti wa CCM na katibu wake wajiuzulu uongozi Reviewed by Zero Degree on 9/05/2017 11:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.