Loading...

Pogba kukaa nje kwa wiki 6 kufuatia majeraha aliyopata kwenye mechi dhidi ya FC Basel


Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba huenda akakaa nje ya uwanja kwa kati ya mwezi mmoja na wiki sita baada yake kuumia misuli ya paja wakati wa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Basel Jumanne.

Mfaransa huyo wa miaka 24 alifanyiwa uchunguzi kuhusu jeraha hilo Jumatano.

Inafahamika kwamba Pogba atakosa kucheza angalau kwa mwezi mmoja.

Hilo lina maana kwamba huenda atakuwa na kibarua kujaribu kuwa sawa kucheza mechi ya Ligi ya Ligi Kuu dhidi ya Liverpool ugenini Tarehe 14, Oktoba.

Meneja wa United Jose Mourinho anatarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu hali yake katika kikao na wanahabari siku ya Ijumaa.

Pogba atakosa mechi za ligi dhidi ya Everton, Southampton na Crystal Palace, pamoja na mechi ya Kombe la Ligi raundi ya tatu siku ya Jumatano dhidi ya Burton.

Kadhalika, ataikosa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ugenini dhidi ya CSKA Moscow mnamo 27 Septemba.

Aidha, atakosa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Bulgaria na Belarus mapema mwezi Oktoba.

Ufaransa wanahitaji kushinda mechi hizo ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka ujao.
Pogba kukaa nje kwa wiki 6 kufuatia majeraha aliyopata kwenye mechi dhidi ya FC Basel Pogba kukaa nje kwa wiki 6 kufuatia majeraha aliyopata kwenye mechi dhidi ya FC Basel Reviewed by Zero Degree on 9/14/2017 08:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.