Loading...

Nape ahoji kuhusu vigezo vya upatikanaji wa watendaji wa vyama vya ushirika


Naibu Waziri wa Killimo, Mifugo na Uvuvi Tate Ole Nasha amewataka watendaji wote wa vyama vya ushirika kufanya kazi kwa uadilifu ili kuhakikisha wanaondoa kero za wakulima na sio kuongeza kero kwa kundi hilo ambalo ni wazalishaji wakuu wa Korosho.

Mh. Ole Nasha ametoa kauli hiyo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtama Mh. Nape Nnauye ambaye alihoji juu ya vigezo vya kupatikana kwa watendaji wa vyama vya ushirika nchini (TCDC) kupitia mfumo wa ushindani kuliko ilivyo sasa ambapo vigezo vilivyopo havina ushindani.

Naibu huyo amesema kuwa sifa za upatikanaji wa watendaji wa vyama vya ushirika zinajitosheleza ambazo ni kuanzia elimu ya kidato cha Nne na kuendelea hivyo kama kuna uzembe unafanyika ni kukosa uadilifu kwa viongozi hao na sio suala la elimu kama inavyodaiwa.

Mh. Nape amekuwa akilalamikia suala la wananchi wa Lindi na Mtwara kutofaidika na zao la Korosho ilihali ndio zao lao kuu la biashara.
Nape ahoji kuhusu vigezo vya upatikanaji wa watendaji wa vyama vya ushirika Nape ahoji kuhusu vigezo vya upatikanaji wa watendaji wa vyama vya ushirika Reviewed by Zero Degree on 9/14/2017 08:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.