Loading...

Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 3 mkoani Arusha


Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Mrisho Gambo amesema Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Magufuli anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha kesho kwa ziara ya siku tatu.

Bw Gambo ametoa tarifa hiyo ofisini kwake jijini Arusha ambayo imebainisha kuwa baada ya kuwasili Mh Rais atazindua barabara ya KIA Mererani inayoanzia katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro hadi mji wa Mererani mkoani Manyara.

Kwa mujibu wa Bw Gambo siku ya tarehe 23/09/2017 mh Rais Magufuli anatarajiwa kutunuku kamisheni kwa maafisawa jeshi tukio litakalofanyika katika uwanja wa Shekh Amry Abedi jijini Arusha na amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuhudhuria sherehe hizo.

Sherehe hizo ambazo kwa kawaida hufanyika katika chuo cha maafisa wa jeshi cha TMA kilichoko Monduli kwa mara ya kwanza zinafanyika katika uwanja wa Shekh Amry abedi hatua ambayo ni fursa ya pekee kwa wananchi kuhuduhria
Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 3 mkoani Arusha Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 3 mkoani Arusha Reviewed by Zero Degree on 9/19/2017 04:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.