Loading...

Conte alivyowakuna mashabiki wa Chelsea kwa kauli hii


Mtandao wa London Evening Standard unaripoti kwamba, Antonio Conte alipendekeza kwamba wachezaji wenye umri mdogo wapewe nafasi kubwa kwenye mchezo wa Chelsea dhidi ya Nottingham Forest utakaochezwa siku ya Jumatano.

Jose Mourinho alijikuta akipata upinzani mkubwa kwa kutotaka kuwapa nafasi wachezaji wenye umri mdogo kipindi alipokuwa Stamford Bridge, lakini Conte anaoknekana kuwa na mtazamo tofauti juu ya hilo.

Licha ya wachezaji kama Nathaniel Chalobah na Nathan Ake kuhamia kwingine kutafuta nafasi ya kutosha uwanjani, na Andreas Christensen kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza baada ya miaka miwili yenye mafanikio akiwa na Borussia Monchengladbach.

Conte amepata fursa ya kuwapa nafasi dimbani vijana wake wenye umri mdogo kuonyesha uwezo wao katikati ya wiki hii Chelsea itakapoivaa Nottingham Forest kwenye kombe la EFL, na inaonekana kama ndio muda pekee anaoutegemea kwa jaribio hilo.

Mtandao wa 'The London Evening Standard' ulimnukuu muitaliano huyo ambaye alisema kitu ambacho mashabiki wengi wa Chelsea walitegemea kukisikia:

“Nafikiri ni muda mzuri kuona kile ambacho wanaweza kufanya vijana wadogo ambao tunashiriki nao kwenye mazoezi kila siku. Wanastahili kupewa nafasi hiyo na nitalitilia maanani.”
Conte alivyowakuna mashabiki wa Chelsea kwa kauli hii Conte alivyowakuna mashabiki wa Chelsea kwa kauli hii Reviewed by Zero Degree on 9/19/2017 03:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.