Loading...

Roman Abramovich alimzuia Conte kusajili hawa wachezaji


Kwa mujibu wa ripoti mablimbali, mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roma Abramovic alikataa kutoa ruhusa ya kuwasajili wachezaji wanne wenye uzoefu.

Licha ya kwamba meneja wa Chelsea, Antonio Conte alikuwa na matamanio makubwa ya kuwasajili wachezaji hao katika majira haya ya joto, bosi huyo wa Chelsea alizuia uhamisho wa Leonardo Bonnuci, Claudio Marchisio (Juventus), nyota wa Swansea, Fernando Llorente na Antonio Candreva wa Inter milan ambao walionekana kuwa na umri mkubwa zaidi.

Ripoti zinadai kuwa, Conte alihitaji kuwasajili wachezaji hao ikiwa ni pamoja na kwamba alishawahi kufanya nao kazi kabla na akahisi Chelsea inahitaji kuwa na wachezaji wa aina hiyo kwa ajili ya kuongeza watu wenye uzoefu zaidi ili kulinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza.

Inaonekana Abramovich anamtaka Conte na benchi lake la ufundi wasajili wachezaji chipukizi (wenye umri mdogo). Kama vile Tiemoue Bakayoko (23) aliyetokea Monaco, Alvaro Morata (24) aliyetokea real Madrid, Zappacosta (25) aliyetokea Torino, na Antonio Rudiger (24) aliyetokea Roma, wote hao wakiwa na umri unaoanzia miaka 25 na kushuka chini, wakati mchezaji pekee mwenye umri mkubwa aliyesajiliwa na Chelsea ni Willy Caballero (35) ambaye alikuwa kama mchezaji huru.
Roman Abramovich alimzuia Conte kusajili hawa wachezaji Roman Abramovich alimzuia Conte kusajili hawa wachezaji Reviewed by Zero Degree on 9/06/2017 12:12:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.