Loading...

Video: Messi atupia manne Barcelona ikiibuka na ushindi wa goli 6-1 kwenye La Liga


Lionel Messi alifunga mabao manne na kuwasiadia viongozi wa La Liga Barcelona kuendeleza rekodi yao ya kushinda mechi zote msimu huu kwa kuandikisha ushindi mkubwa dhidi ya Eibar.

Messi alifunga mkwaju wa penalti na kuwaweka wenyeji hao kifua mbele kabla ya Paulinho kufunga la pili kwa kichwa.

Denis Suarez kisha alifunga kutoka kwa mpira wa kudunda lakini Sergi Enrich akawakombolewa Eibar bao moja na kufanya mambo kuwa 3-1.

Messi alifunga mabao mawili katika muda wa dakika moja kabla ya kubadilishana pasi murua na Aleix Vidal na kufunga bao lake la nne dakika za mwisho kwenye mechi hiyo.

Ushindi huo unawaweka Barcelona uongozini wakiwa na alama 15, alama tano mbele ya Sevilla walio wa pili ingawa Barca wamecheza bao moja zaidi.

Messi kwa mara nyingine anaonekana kung'aa mbele ya wavu.

Mshambuliaji huyo wa Argentina amefunga mabao tisa mechi zake nne za karibuni La Liga.

Bao lake la nne Jumanne limefikisha 301 idadi ya mabao ambayo amefunga Nou Camp katika kipindi cha miaka 13.


Mshambuliaji wa zamani wa West Ham Simone Zaza naye alifunga mabao matatu katika kipindi cha dakika tisa na kuwasaidia Valencia kulaza Malaga 5-0.

Video: Messi atupia manne Barcelona ikiibuka na ushindi wa goli 6-1 kwenye La Liga Video: Messi atupia manne Barcelona ikiibuka na ushindi wa goli 6-1 kwenye La Liga Reviewed by Zero Degree on 9/20/2017 09:01:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.