Loading...

Wayne Rooney afungiwa kuendesha gari kwa miaka miwili


Nahodha wa zamani wa kikosi cha England Wayne Rooney amefika mahakamani na kukiri kuendesha gari akiwa mlevi.

Alikamatwa wakati polisi walisimamisha gari lake huko Wilmslow, Cheshire tarehe mosi mwezi Septemba.

Rooney 31 alipigwa marufuku ya kuendesha gari kwa miaka miwili na kuamrishwa kutoa huduma ya jamii bila malipo kwa masaa 100.

Rooney pia aliamrishwa kulipa pauni 170 wakati alipofika katika mahakama ya Stockport.

Mzaliwa huyo wa Liverpool aliyejiunga tena na klabu yake ya utotoni ya Eveton miaka 13 tangu ahame na kuelekea Manchester United.

Baba huyo wa watoto watatu ndiye anayeshikiria rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi nchini Uingereza.
Wayne Rooney afungiwa kuendesha gari kwa miaka miwili Wayne Rooney afungiwa kuendesha gari kwa miaka miwili Reviewed by Zero Degree on 9/18/2017 03:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.