Loading...

Yanga wafunguka kuhusu hatima ya Kocha George Lwandamina


BAADA ya kuzagaa kwa taarifa za Klabu ya Yanga kupanga kuachana na kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, ameibuka na kuweka wazi hatima ya kocha huyo ndani ya kikosi hicho.

Taarifa za mwanzo ambazo zilikuwa zinasambaa zilidai kuwa Yanga wamempa mechi tano Lwandamina kama kipimo kabla ya kuachana naye kutokana na matokeo mabaya ambayo wamekuwa wakiyapata kwenye mechi zao za hivi karibuni.

Gazeti la Championi linadai kwamba, Sanga amesema kuwa uongozi wao hauna nia yoyote ya kumfungashia virago Lwandamina raia wa Zambia kama baadhi ya watu ambavyo wamekuwa wakizusha juu yao kutaka kumtimua kocha huyo.

“Wala siyo kweli, kama ingekuwa kweli basi ningekwambia, lakini pia labda watu waseme mitaani, unajua watu wanasema kwa kuwa Simba wao walimpa kocha wao mechi tano, wanataka kuonyesha Yanga nao wamefanya hivi.

“Kwa mfano hiyo pafomansi unaipima vipi kwa mazingira yaliyopo kusema kweli, lakini hatujaamua wala kikao cha jana (juzi) hatujaongelea jambo hilo na wala hakijahusisha hata kidogo masuala hayo,” alisema Sanga.
Yanga wafunguka kuhusu hatima ya Kocha George Lwandamina Yanga wafunguka kuhusu hatima ya Kocha George Lwandamina Reviewed by Zero Degree on 9/18/2017 04:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.