Loading...

Zitto akamatwa Uwanja wa Ndege Jijini Dar


Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT –Wazalendo), Zitto Kabwe amekamatwa na polisi akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Kigoma.

Ofisa Habari wa ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis amesema Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa chama hicho amekamatwa jioni hii.

Jana Jumatano asubuhi, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema Zitto atafutwe, akamatwe na kufikishwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Alisema Zitto alipewa barua ya wito wa kufika mbele ya kamati hiyo baada ya Spika Job Ndugai kuagiza hilo lifanyike lakini hajalitekeleza.
Zitto akamatwa Uwanja wa Ndege Jijini Dar Zitto akamatwa Uwanja wa Ndege Jijini Dar Reviewed by Zero Degree on 9/21/2017 08:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.