Mzee Akilimali afunguka mazito kuhusu migomo ya wachezaji Yanga
Katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahimu Akilimali |
Mzee Akilimali amesema wamegundua mgomo uliotokea hapo jana kwa wachezaji kutohudhuria mazoezi ni njama iliyopangwa na Sanga wakidai kuwa wachezaji hawajalipwa mishahara yao suala ambalo sio sawa.
Mzee Akilimali amesema siku moja kabla ya mazoezi alionekana Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Sanga akiwa na Nahodha wa Timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' pamoja na Mshambuliaji wa Kimataifa Thaban Kamusoko ambapo baada ya kutoka hapo timu ikasema haijapata mshahara wa mwezi uliopita pamoja na mwezi huu hivyo wanaamua kugoma suala ambalo amesema ni njama.
"Mimi naona tu kwamba Sanga sasa imefikia hapa, ili tufanye vizuri nawasihi Watanzania wote hususani wana Yanga na wapenzi wa Yanga bwana Sanga sasa hivi atamke kujiuzulu, chonde chonde Bwana Sanga iache Yanga watu tuketi pamoja na wewe mwenyewe tuchague viongozi Yanga tusonge mbele" amesema Mzee Akilimali.
Mzee Akilimali amesema siku moja kabla ya mazoezi alionekana Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Sanga akiwa na Nahodha wa Timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' pamoja na Mshambuliaji wa Kimataifa Thaban Kamusoko ambapo baada ya kutoka hapo timu ikasema haijapata mshahara wa mwezi uliopita pamoja na mwezi huu hivyo wanaamua kugoma suala ambalo amesema ni njama.
Akilimalia anadai kuwa Sanga amewataka wachezaji kutokusikiliza maneno ya baadhi ya viongozi ambayo yanalenga kurudisha nyuma maendeleo ya Klabu kwani Klabu hiyo itakaposhindwa kufanya vizuri lawama zote zitaangukia kwa Klabu wakiwemo viongozi.
"Kama Yanga ikifanya vibaya hivi sasa na mpaka ikafikia hatua ya kushuka daraja hivi atalaumiwa nani na hasara ya nani? Mimi niwaonye wachezaji kwamba sio vizuri wala sio nidhamu kugomea mazoezi,mtu hagomei mazoezi bali anagomea mchezo, hata kama unadai mwezi wa kwanza, wapili, watatu wewe mazoezini nenda kwasababu unajiweka tayari wakikulipa waajiri wako lazima ukatekeleze kazi yao, sasa leo unagomea mazoezi pesa watatafuta wanakupa, unakwenda kukutana na Ndanda FC unafungwa, utawaambiaje waajiri wako, kama pesa wameshakulipa" alisema Mzee Akilimali.
Mzee Akilimali afunguka mazito kuhusu migomo ya wachezaji Yanga
Reviewed by Zero Degree
on
9/21/2017 09:01:00 AM
Rating: