Loading...

49% ya akinamama wajawazito wako hatarini kupoteza maisha


Asilimia 49 ya akinamama wajawazito wanaoishi maeneo ya vijijini katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi, wako kwenye hatari ya kupoteza maisha wakati wa kujifungua, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujifungulia majumbani na upungufu wa wauguzi na wakunga wenye ujuzi na weledi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Takwimu hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto Mh. Dk. Faustine Ndugulile katika uzinduzi wa mradi wa More and Better Midwives for Rural Tanzania unaolenga kuongeza idadi ya wakunga na kuwafanya wawe bora, huku akitumia fursa hiyo kukemea vitendo vya rushwa na lugha zisizo za staha zinazodaiwa kutolewa na baadhi ya wauguzi kwa wagonjwa.

Mratibu wa mafunzo ya afya Kanda ya Ziwa Dk. Hyasinta Jaka, anaeleza changamoto wanazozipata katika kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga, huku Msajili wa Baraza la uuguzi na ukunga nchini Lena Mfalila akiwataka wauguzi kufanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia maadili ya taaluma yao.

Naye Mkurugenzi mkazi wa JHPIEGO Tanzania Jeremie Zoungrana, anasema ili kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto, ni muhimu kuwa na wauguzi na wakunga wenye weledi ili kuboresha mazingira ya uotaji wa huduma bora za afya nchini.

Mradi huo wa miaka mitano unaofadhiliwa na serikali ya canada na kutekelezwa na shirika la JHPIEGO kwa ushirikiano na AMREF na Chama cha wakunga Canada kupitia chama cha wakunga Tanzania pia utatoa ufadhili kwa wanafunzi wa Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi wanaojiunga na vyuo vya uuguzi na ukunga wasio na uwezo wa kulipa ada pamoja na mahitaji mengine.

Source: ITV
49% ya akinamama wajawazito wako hatarini kupoteza maisha 49% ya akinamama wajawazito wako hatarini kupoteza maisha Reviewed by Zero Degree on 10/19/2017 11:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.