Loading...

Mrithi wa Mayanja atambulishwa rasmi Simba SC

Irambona Masoud Djuma (katikati)
BAADA ya kupita siku moja tangu kocha msaidizi wa timu ya Simba, Jackson Mayanja, raia wa Uganda aamue kujiweka pembeni kukinoa kikosi hicho, hatimaye uongozi wa timu hiyo umemalizana na aliyekuwa kocha wa Rayon Sport ya Rwanda, Irambona Masoud Djuma, kwa ajili ya kubeba mikoba ya Mganda huyo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo, Djuma aliweka hadharani kuwa amekuja katika kikosi hicho kwa ajili ya kufanya kazi na kukisaidia kufanya vizuri kwenye kila kombe watakaloshiriki.

“Nimekuja hapa Simba kwa ajili ya kaufanya kazi tu, na nataka tushirikiane ili timu iweze kusonga mbele itoke hapa ilipo, na pia nipo hapa ili kukuza jina langu maana kiukweli unapozungumzia Simba unazungumzia juu ya klabu kubwa hapa nchini,” alisema kocha huyo.

Lakini pia uongozi wa Simba chini ya Kaimu Rais wake, Salim Abdallah ‘Try Again’, umemteua Richard Robert kuwa meneja wa kikosi hicho akichukua mikoba ya Cosmas Kapinga ambaye aliamua kubwaga manyanga hivi karibuni.
Mrithi wa Mayanja atambulishwa rasmi Simba SC Mrithi wa Mayanja atambulishwa rasmi Simba SC Reviewed by Zero Degree on 10/19/2017 11:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.