Loading...

FIFA yaitolea nje Leicester City


Fifa imekata ombi la FA la kutaka idhini ya mchezaji wa kiungo cha kati Adrien Silva kujiunga na Leicester City kutoka Sporting Lisbon.

Leicester iliwasilisha stakabadhi za kuhama kwa Silva kwa kima cha pauni milioni 22, wakiwa wamechelewa kwa sekunde 14 wakati wa siku ya kukamilika tarehe ya kuhama wachezaji tarehe 31 mwezi Agosti

Sasa Leicester wataweza kumjumuisha Silva kwa kisosi chao wakati wa kuanza tena msimu wa wachezaji kuhama mwezi Januari.

Silva alirudi katika uga wa Estadio Jose Alvalade siku ya Jumapili, kuwapa kwaheri mashabiki ya klabu yake ya zamani kabla ya sare ya 0-0 na mahasimu Porto.

Alirejea uUeno mwezi uliopita kujiunga na famalia yake.

Leicester ambao kwa sasa wako nafasi 17 katika Premier League kwa ushindi mmoja tu msimu huu, walimuuza Danny Drinkwater kwenda Chelsea kwa pauni milioni 35 huku Silva akitarajiwa kuchukua nafasi yake.
FIFA yaitolea nje Leicester City FIFA yaitolea nje Leicester City Reviewed by Zero Degree on 10/04/2017 04:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.