Takukuru wafunguka kuhusu ushahidi wa Rushwa Arusha
Aidha, taasisi hiyo imemtaka mbunge huyo kuwasilisha nyaraka zaidi baada ya yeye na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, kuwasilisha flashi walizodai zina video ya madai yao juzi.
Akifuatana na Lema na Mch. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini, Nassari (31) aliwasilisha flashi hizo anazodai kuwa zina ushahidi makao makuu ya Takukuru jijini Dar es Salaam.
Mussa Misalaba, Ofisa Uhusiano na Habari wa Takukuru, aliiambia Nipashe jana kuwa Nassari na wabunge wenzake waliwasilisha ushahidi wao juzi wakidai una taarifa za madiwani waliohama Chadema kujihusisha na rushwa ya uongozi wa wilaya na mkoa.
Misalaba alisema Takukuru iliwapokea wabunge hao na kuwaelekeza kuwasilisha kwake vielelezo vya ziada vinavyoonyesha ushahidi zaidi wa tukio hilo.
Ofisa huyo wa Takukuru alisema ingawa waliwataka wabunge hao kupeleke vielelezo zaidi, taasisi yake ilishaanza kulifanyia uchunguzi suala hilo tangu ilipopokea vielelezo vya awali juzi.
Kutokana na maelezo hayo ya Misalaba, Nipashe ilimtafuta Nassari kwa simu kujua sababu za kutowasilisha vielelezo vingine katika ofisi ya Takukuru jana kama alivyoahidi juzi na akasema alishindwa kutokana na nyaraka hizo kuwa jijini Arusha ilhali yeye yuko Dar es Salaam.
Alisema nyaraka hizo alitarajia kuzipokea kutoka Arusha jana jioni na ataziwasilisha Takukuru leo.
Wiki iliyopita Nassari na Lema waliahidi kupeleka ushahidi Takukuru wenye video ya madai yao ya madiwani wawili wa Chadema kupewa rushwa na baadhi ya viongozi wa serikali mkoani Arusha ili wakihame chama chao na kujiunga na CCM.
Walidai madiwani hao ni waliotangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi wakati wa hafla ya kukabidhi kamisheni kwa maofisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) jijini Arusha.
Wabunge hao waliomba kuwasilisha ushahidi huo katika ofisi za Takukuru ili viongozi wa serikali waliohusika na njama hizo wachukuliwe hatua za kisheria.

"Ni kweli walileta ushahidi kwenye CD," Misalaba alisema, "sasa hatuwezi kutegemea ushahidi huo tu. Tumewapa maelekezo ya kuleta vielelezo vingine."
"Na walitakiwa kuleta leo (jana) lakini hawajaja, ila bado tunasubiri."
Kutokana na maelezo hayo ya Misalaba, Nipashe ilimtafuta Nassari kwa simu kujua sababu za kutowasilisha vielelezo vingine katika ofisi ya Takukuru jana kama alivyoahidi juzi na akasema alishindwa kutokana na nyaraka hizo kuwa jijini Arusha ilhali yeye yuko Dar es Salaam.
Alisema nyaraka hizo alitarajia kuzipokea kutoka Arusha jana jioni na ataziwasilisha Takukuru leo.
Wiki iliyopita Nassari na Lema waliahidi kupeleka ushahidi Takukuru wenye video ya madai yao ya madiwani wawili wa Chadema kupewa rushwa na baadhi ya viongozi wa serikali mkoani Arusha ili wakihame chama chao na kujiunga na CCM.
Walidai madiwani hao ni waliotangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi wakati wa hafla ya kukabidhi kamisheni kwa maofisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) jijini Arusha.
Wabunge hao waliomba kuwasilisha ushahidi huo katika ofisi za Takukuru ili viongozi wa serikali waliohusika na njama hizo wachukuliwe hatua za kisheria.
Takukuru wafunguka kuhusu ushahidi wa Rushwa Arusha
Reviewed by Zero Degree
on
10/04/2017 04:00:00 PM
Rating: