Loading...

Atletico Madrid yazipiku Arsenal, Liverpool kwa nyota huyu


Atletico Madrid wameafikiana "makubaliano ya awali" ya kumchukua winga wa Monaco Thomas Lemar ambaye alikuwa akitafutwa sana na Arsenal kabla ya kuondoka kwa Arsene Wenger.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa - ambaye amekaa misimu mitatu tangu kuwasili Monaco akitokea Caen, kwa sasa yupo Urusi kucheza michuano ya Kombe la Dunia.

Arsenal walishindwa kumnunua Lemar, 22, kipindi cha kuhama wachezaji majira ya joto mwaka jana.
Alikuwa pia akitafutwa na Liverpool waliotaka kulipa £60m.

"Katika siku zinazofuata, klabu hizi mbili sasa zitafanya juhudi kukamilisha uhamisho huo," Atletico wamesema.
Lemar amefunga mabao 22 katika mechi 123 alizochezea Monaco na aliwasaidia kushinda Ligue 1 na kufika nusufainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu wa 2016-17.

Alichezea timu ya taifa ya Ufaransa mara ya kwanza 2016 na amewafungia mabao matatu katika mechi 12 alizowachezea tangu wakati huo.
Atletico Madrid yazipiku Arsenal, Liverpool kwa nyota huyu Atletico Madrid yazipiku Arsenal, Liverpool kwa nyota huyu Reviewed by Zero Degree on 6/13/2018 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.