Atletico Madrid yakamilisha usajili wa kiungo huyu
Licha ya kushinda taji la Ligi ya Europa, Diego Simeone anataka kuongeza nguvu mpya katika kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao kwa lengo la kuleta changamoto kwenye mbio za kuwania Ubingwa. Kuboresha safu ya kiungo ilikuwa ni moja ya mipango yake na amekuwa akimvizia nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa muda mrefu.
Nyota huyo alianza kuonekana akiwa na Atletico lakini aliachwa mwaka 2013 kwa sababu ya kukosa nguvu. Alijiunga na Villarreal na kucheza mchezo wake wa kwanza mkubwa akiwa na klabu hiyo mwaka 2015 na kuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi cha kwanza katika msimu uliofuata, akicheza mechi 31.

Mhispania huyo, ambaye anacheza kama kiungo mkabaji, amekuwa miongoni mwa wachezaji walioanza na kikosi cha kwanza mara kwa mara katika klabu hiyo msimu huu wa 2017/18 , akifunga goli 1 na kutoa 'assist' 4 ndani ya mechi 47 katika michuano yote na kuisaidia klabu kumaliza ligi katika nafasi ya tano kwenye msimamo.
Ni kiungo mwenye kipaji kikubwa, anaweza kujitengenezea nafasi uwanjani na kucheza kwa bidii. Ana uwezo mkubwa kwenye swala la kurejesha mpira upande wao pale unapokuwa umepotea na amefanya hivyo katika msimu huu wa 2017/18 mara 320 kwa timu yake, na kuandika historia kwenye LaLiga.
Rodri pia anaweza kumiliki mpira na alikuwa mchezaji watatu mwenye kiwango kikubwa cha pasi zilizofanikiwa. (2,470).
Ameshinda taji la michuano ya Euro U19 akiwa na Uhispania mwaka 2015 na amekuwa mchezaji wa kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Uhispania U21. Alicheza mechi yake ya kwanza kubwa akiwa na Uhispania dhidi ya Ujerumani mwezi Machi.

Reviewed by Zero Degree
on
5/24/2018 06:20:00 PM
Rating: