Loading...

Tarehe ya Paul Pogba kurejea uwanjani


Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba anatarajiwa kurejea mwezi ujao wakati mashetani wekundu watakaposhuka dimbani kuikabili Chelsea.

Mfaransa huyo amekaa benchi tangu septemba 12 kufuatia majeraha aliyopata kwenye paja wakati Man United ilipocheza dhidi ya FC Basel kwenye Ligi ya Mabingwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya L'Equipe, hali ya Pogba sasa inaendelea vizuri kuliko awali na anategemewa kurejea kwenye Ligi Kuu, tarehe 5 Novemba, Manchester United itakaposhuka kwenye dimba la Stamford Bridge kucheza na Chelsea.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 bado hajarejea mazoezini rasmi na Man United watafanya maamuzi ya kumzuia kuiwakirisha Ufaransa kwenye mechi za kirafiki dhidi ya Wales na Ujerumani.

Kwa uhakika zaidi, Pogba anategemewa kuwa vizuri zaidi Manchester United itakapoikaribisha Newcastle Old Traford, tarehe 18 Novemba.

Manchester United walifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya Carabao baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Swansea.


Mourinho alisema: "Tulikuwa katika hali nzuri na tulicheza kwa ufundi kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho.

“Umakini wa kutosha, mchezo ulikuwa chini ya uwezo wetu, pia ninafurahi kwa matokeo tuliyopata na viwango walivyoonyesha wachezaji.

“Kwa ujumla tulitawala mchezo.”

Manchester United wataikaribisha Tottenham siku ya Jumamosi, wakitazamia kupunguza utofauti wa pointi uliopo kati yao na vinara wa Ligi Kuu.
Tarehe ya Paul Pogba kurejea uwanjani Tarehe ya Paul Pogba kurejea uwanjani Reviewed by Zero Degree on 10/26/2017 09:34:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.