Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 26 Octoba, 2017


Mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Asamoah Gyan, 31, ambaye anaichezea klabu ya Uturuki ya Kayserispor, anatarajiwa kuanzisha kampuni yake ya ndege baada ya kupata leseni ya biashara hiyo nchini Ghana.

Mshambuliaji wa West Ham Angelo Ogbonna hakuamini baada ya timu hiyo kuwashangaza wachezaji wa Spurs kwa kutoka nyuma 2-0 na kubadili matokeo kuwa 3-2 na kufuzu katika robo fainali ya kombe la Carabao.

Lakini je alisahau kwamba tayari wako katika uwanja wa Wembley.

Arsenal na Manchester City zinaweza kulazimika kucheza mechi za marejeleo ya kombe la EFL raundi ya nne baada ya kuwatoa na kuwaingiza wachezaji wengi katika kipindi cha lala salama.

Wamiliki wa ardhi katika uwanja wa West Ham wako katika hatari ya kufilisika , huku West Ham wakiwa katika hatari ya kufurushwa katika uwanja huo.

Newcastle na West Brom wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Wolves' ,24, Conor Coady.(Sun)

Barcelona bado wanaendelea na mkakati wa kutaka kumsajili Philippe Coutinho mnamo mwezi wa Januari, huku Liverpool ikiweka thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kuwa £133m. (Mundo Deportivo).

Tottenham wanamsaka kiungo wa kati wa Ajax Donny van de Beek, 20, na kinda mwenye umri wa miaka 18- Justin Kluivert, mwanawe mshambuliaji wa zamani wa Uholanzi Patrick. (Sky Sports)


Arsenal na Manchester United wote wanamchunguza mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund', 28, Marco Reus, ambaye kandarasi yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu (Sky Germany, kupitia Daily Mail)

Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw, 22, ana wasiwasi kwamba huenda asipate fursa ya kuichezea klabu hiyo baada ya uhusiano wake na meneja Jose Mourinho kuharibika. (Guardian)

Shaw na Mourinho wanadaiwa kutozungumziana kufuatia madai ya beki huyo wa kushoto kwamba hachezeshwi msimu huu. (Times)

Arsenal wanamtaka aliyekuwa mkurugenzi wa Barcelona Raul Sanllehi, ambaye alihusika katika kumsajili Neymar kuja kuwa kama mkurugenzi wao mpya wa michezo.(Sport)

Winga wa zamani wa Arsenal Marc Overmars, ambaye sasa ni mkurugenzi katika klabu ya Ajax pia ni mgombea mwengine wa wadhfa huo. (Independent)

Kroenke anasema kuwa hatoiuza klabu hiyo na anapanga kuirithisha familia yake umiliki huo. (Mirror)

Mashabiki wa Arsenal hawataki mwana wa Kroenke Josh na mwenyekiti wa Sir Chips Keswick waajiriwe katika bodi ya wakurugenzi. (Daily Mail)

Mauricio Pochettino anadai Daniel Levy hawawekei viwango vya umri wachezaji wanaosainiwa na Tottenham licha ya klabu hiyo kuwapendelea wachezaji wachanga wakati inapoingia katika soko. (London Evening Standard)

Beki wa Crystal Palace Pape Souare alibahatika baada ya tisheti yake aliyowarushia mashabiki kurudishwa na shabiki aliyeipata.

Mmiliki wa Arsenal, Stan Kroenke anasema kuwa klabu hiyo haijafa moyo wa kuwabakiza kikosini, kiungo wakati Mesut Ozil, 29, na mshambuliaji Alexis Sanchez, 28. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 26 Octoba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 26 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/26/2017 02:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.