Loading...

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez avunja ukimya kuhusiana na suala la Harry Kane


Rais wa Real Madrid, Florentino Perez azungumzia mapenzi waliyonayo kwa mshambuluaji wa Tottenham, Harry Kane.

Harry Kane akipeana mkono na Cristiano Ronaldo wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa kati ya Real Madrid na Tottenham
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza alikuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki Bernabeu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Real Madrid na Tottenham, huku kukiwa na tetesi zinazosambaa kwa kasi zikidai Real Madrid itajaribu kumsajili nyota huyo katika kipindi cha majira ya joto.

Kane amefanikiwa kujitengezea jina na kuwa mmoja wa washambuliaji bora duniani katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, akifunga magoli 31 katika msimu wa 2014/15, 29 msimu wa 2015/16 na magoli 35 msimu uliopita.

Tayari ana magoli 13 katika mechi 12 alizocheza msimu huu, lakini Perez anasistiza kwamba, nyota huyo hayuko kwenye mipango ya klabu hiyo.

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez
"Suala la kumsajili Harry Kane bado halijaingia katika kichwa changu. Kweli ni mchezaji mzuri na bado ni mdogo kiumri," Perez aliiambia 'Cadena COPE'.

"Bado ana miaka mingi ya kuendeleza kipaji chake, lakini tunafurahia uwepo wa Karim Benzema na wengine wengi.

"Sikumuuliza Rais wa Tottenham juu ya dau la Kane kwa sababu angeniambia ana thamani ya euro milioni 250."

Tottenham watakutana tena na Real Madrid katika dimba la Wembley wiki ijayo kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa baada ya mchezo wao wa Carabao dhidi ya West Ham siku ya Jumatano na wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Manchester United wikendi ijayo.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez avunja ukimya kuhusiana na suala la Harry Kane Rais wa Real Madrid, Florentino Perez avunja ukimya kuhusiana na suala la Harry Kane Reviewed by Zero Degree on 10/25/2017 10:26:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.