Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 25 Octoba, 2017

Marco Reus
Manchester United na Arsenal wanamfuatilia nota wa klabu ya Borussia Dortund, Marco Reus.(Sky Sports)

Michael Appleton anatarajiwa kuacha wadhifa wa kaimu meneja wakati Leicester wanakaribia kumteua aliyekuwa maneja wa Southmpton Claude Puel. (Daily Telegraph)
Mesut Ozil
Manchester United haijachukua hatua ya kumpata mshambuliaji wa Arsenal Mesut Ozil, lakini ni kati ya vilabu vitatu ambavyo mchezaji huyo wa miaka 29 raia wa Ujerumani angepenada kuhamia akitoka Arsenal. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji raia wa Senegal Diafra Sakho, 27, anasema anataka kuondoka West Ham. (Claude Atcheba)

Charly Musonda, 21
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amekana madai kuwa mchezaji wa safu ya kati Charly Musonda, 21, anaruhusiwa kukihama klabu hiyo mwezi Januari kwa mkopo. (Daily Express)

Ajenti wa mchezaji wa kiungo cha kati wa Southampton Sofiane Boufal, 24, anadai vilabu vya Italia vya Fiorentina na Inter Milan vilitaka kumsaini. (SFR Sport)

Aliyekuwa meneja wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel, 44, hajakataa ikiwa atakubali kuwa meneja wa Everton ikiwa ataombwa kufanya hivyo.

Meneja wa West Ham amekataa kulaumu kusainiwa wachezaji wapya baada ya kushindwa nyumbani na Brighton Ijumaa iliyopita. (Evening Standard)

Marekani inatathmini miji ambayo inaweza kuomba kuandaa kombe la dunia mwaka 2016. (Washington Post)

Crystal Palace wana nia ya kumsaini Danny Ings, 25, kutoka Liverpool kwa mkopo mwezi Januari lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa vilabu vingine vitatu. (News Shopper)

Harry Kane, 24
Rais wa Real Madrid Florentino Perez anasema kuwa itagharimu pauni milioni 223 kumnunua mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza, Harry Kane, 24. (Calciomercato)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 25 Octoba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 25 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/25/2017 11:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.