Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 12 Octoba, 2017


Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Bercelona Oscar Grau anasema kuwa klabu hiyo itajaribu tena kumsajili kiungo wa Brazil Philippe Coutinho, 25, wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari.

Kipa wa zamani wa Liverpool na Wigan Athletic Chris Kirkland amezungumza kuhusu makabiliano yake na ugonjwa wa shinikizo la kiakili akisema kuwa ugonjwa huo ulimshinikiza kustaafu. (Chanzo: Guardian)

Liverpool itaendelea kukataa kuingia katika makubaliano ya kumuuza Coutinho Barcelona.

Mazungumzo ya kuuongeza mkataba wa Mesut Ozil Arsenal yanaendelea kwa njia nzuri kulingana na ajenti wa kiungo huyo wa kati wa Ujerumani.

Palace Itapinga ombi lolote jipya kutoka Leicester kumunua mchezaji mwenye umri wa 26, Andros Townsend. (Chanzo: Independent)

Vilevile , Liverpool imekubali kumkubali Coutinho kuelekea Nou Camp mnmao mwezi Januari katika makubaliano yenye thamani ya £98.6m. (
Chanzo: Mundo Deportivo kupitia Daily Mail)

Meneja Jose Mourinho yuko tayari kutia saini kandarasi ya miaka mitano na klabu ya Manchester United itakayokuwa na thamani ya £65m 


Palace huenda inajiandaa kumuuza mchezaji wa Uingereza Townsend kwa Leicester ili kuisaidia katika ununuzi wa mshambuliaji bora.(Chanzo: Sun)

Mchezaji wa Manchester United Juan Mata, 29, amekataa fursa ya kuhamia katika ligi ya China

Kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere, 25, anaaminika kutaka kuondoka Arsenal mwezi Januari ili kuimarisha uwezo wake wa kujumuishwa katika kikosi cha kombe la dunia cha kocha Gareth Southgate (Chanzo: Daily Mirror)

Beki wa kulia wa Paris St-Germain Dani Alves amesema kuwa itakuwa bora iwapo klabu yake itamsajili mshambuliaji Alexis Sanchez , 28, ambaye kandarasi yake Arsenal inakamilika mwisho wa msimu huu. (Chanzo: Cooperativa)

Bristol City ni miongoni mwa timu nne za Uingereza zinazomsaka winga wa MotherwellAdam Livingstone. (Chanzo: Motherwell Times)

Chelsea wanahofia kiungo wa kati wa Ufaransa N'Golo Kante, 26, huenda akakosa kushiriki katika mechi zote sita za mwezi Oktoba kutokana na jeraha la nyuma ya goti. 

Mshambuliaji wa Colombia Radamel Falcao na kiungo wa kati wa Peru Renato Tapia wamekiri kwamba sare itazisaidia timu zote mbili katika awamu ya mwisho ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia siku ya Jumanne usiku.(Chanzo: Telegraph)

Burnley, Newcastle United na West Brom wanataka kumsajili beki wa Intermilan Yuto Nagamoto(Chanzo: talksport)

Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anawalenga wachezaji wa ligi ya Premia wenye uzoefu mwezi Januari huku akijaribu kuinusuru klabu hiyo kushushwa daraja. 

Tottenham wanatarajiwa kuvunja rekodi ya miaka 10 kushiriki katika ligi ya Uingereza wakati watakapowakaribisha nyumbani Bournemouth katika uwanja wa Wembley siku ya Jumamosi.

Mshambuliaji wa Leicester Ahmed Musa amefungua kituo cha kuuza mafuta nchini Nigeria. (Chanzo: Daily Mail)

Mshambuliaji wa Bournemouth Jermain Defoe anasema kuwa ni ndoto yake kushiriki katika kikosi cha kombe la dunia 2018. (Chanzo: Sky Sports)

Waandishi wa Brazil wamezitaja klabu za Arsenal, Manchester City na Chelsea kuwa miongoni mwa klabu zinazotoa chakula kizuri kwa wanahabari katika taifa ambalo chakula chake sio kizuri sana duniani.. (Chanzo: UOL)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 12 Octoba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 12 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/12/2017 02:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.