Loading...

Wenger: Nafasi ya Wilshere Kombe la Dunia 2018 ni ya uhakika


Arsene Wenger anasema kwamba, Jack Wilshere hahitaji kuondoka Arsenal ili kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha timu yake ya Taifa kwenye michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyikia Urusi.

Wenger anasema, Wilshere anatakiwa abaki Arsenal
Wilshere, ambaye mkataba wake utaisha katika majira ya joto mwakani, amekua akihusishwa na kuondoka Arsenal ili apate nafasi ya kutosha uwanjani na ajitengenezee nafasi ya kuwekwa kwenye mipango ya kocha wa Uingereza, Gareth Southgate kwenye Kombe la Dunia mwaka 2018.

Kiungo huyo ambaye aliichezea Uingereza kwenye Euro 2016, hajaichezea Arsenal kwenye Ligi Kuu ya Uingereza tangu atoke Bournemouth alikokua kwa mkopo.


Akizungumza na 'Sky Sports' kuelekea mechi ijayo ya Jumamosi dhidi ya Watford, Wenger alisema: "Hakuna ulazima wa Wilshere kuondoka Arsenal ili kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia.

"Naamini kwamba, kwa sasa Jack yuko kwenye kiwango kizuri sana, hata mimi binafsi nimejionea.

"Anakaribia kutambuliwa kwa mchango wake, kama wanavyotambuliwa wengineo.

"Nafikiri, kama ataendelea na mwenendo huu alionao sasa, hakika, ataenda kushiriki Kombe la Dunia.

"Sidhani kwamba, Jack atakua kwenye kiwango cha juu na anyimwe nafasi ya kucheza Kombe la Dunia."

"Ameshacheza mechi kadhaa pamoja nasi na yuko kwenye mipango yetu na bado atacheza mechi nyingine nyingi zaidi."
Wenger: Nafasi ya Wilshere Kombe la Dunia 2018 ni ya uhakika Wenger: Nafasi ya Wilshere Kombe la Dunia 2018 ni ya uhakika Reviewed by Zero Degree on 10/12/2017 06:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.