Loading...

Wanafunzi 85 Kanda ya Ziwa wafadhiliwa kusoma nje ya nchi.


Wanafunzi 85 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wamepata udhamini wa masomo ya shahada ya kwanza kwenye fani za udaktari, uhandisi, uchumi, sheria za mitandao na teknolojia ya viwanda katika nchi za China, Canada na Marekani, kupitia taasisi ya Universties Abroad Representative.

Mkurugenzi Mkazi wa Universties Abroad Representative ( UAR )Bw.Tony Kabetha amesema wanafunzi hao wanatakiwa kutambua kuwa taaluma wanazokwenda kuzisomea ndizo zinazopewa kipaumbele hivi sasa kwenye sera ya serikali ya viwanda kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2015, hivyo hawana budi kutanguliza mbele maslahi ya taifa na kujiepusha na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Afisa Elimu wa mkoa wa Mwanza, Mwalimu Michael Ligola amewashauri wazazi na walezi wa wanafunzi hao kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya vijana wao wakati wote wa masomo yao nje ya nchi, huku akiwahimiza wanafunzi hao kuepuka mambo yasiyo ya msingi kwa maisha yao, ikiwemo kujitumbukiza kwenye biashara ya dawa za kulevya pamoja na kuiga tamaduni za nchi za Magharibi.

Baadhi ya wazazi wanaosomesha watoto wao katika fani ya udaktari nchini China, wanatoa ushuhuda wa maisha yalivyo katika nchi hiyo ya Bara la Asia,kwa wanafunzi wanaotarajia kuondoka nchini kuanzia Oktoba 13 na Oktoba 14 mwaka huu.
Wanafunzi 85 Kanda ya Ziwa wafadhiliwa kusoma nje ya nchi. Wanafunzi 85 Kanda ya Ziwa wafadhiliwa kusoma nje ya nchi. Reviewed by Zero Degree on 10/02/2017 06:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.