Loading...

Alichosema Haruna Niyonzima kuhusiana na ishu ya Mavugo kuondoka Simba SC

Laudit Mavugo
Kufuatia tetesi za kutemwa kwa mshambuliaji Timu ya Taifa ya Burundi na Simba SC, Laudit Mavugo, kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mchezaji huyo hawezi kukosa timu kama akiachwa.

Mavugo yumo kwenye orodha ya wachezaji watakaoachwa kwenye dirisha dogo la usajili msimu huu, kisa kikidaiwa kuwa ni kuchuka kwa kiwango chake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gazeti la Championi, Niyonzima alisema Mavugo bado ana uwezo mkubwa sana wa kufunga mabao, lakini anashindwa kutimiza majukumu yake kutokana na mambo madogo madogo.

Niyonzima alisema, mshambuliaji huyo kinachomfanya ashindwe kucheza ni presha kubwa iliyopo kwenye timu huku akimtabiria kuwa akienda kwingine atacheza vizuri.

Taarifa hiyo inadai kwamba, Haruna Niyonzima alisema: “Mavugo siyo mbaya kiasi hicho, binafsi naona ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao katika timu.

“Lakini kitu kikubwa kinachomfanya ashindwe kucheza vizuri ni presha iliyopo katika timu pekee na siyo kitu kingine.

“Ninakuhakikishia akienda timu nyingine tofauti na Simba atakuwa tegemeo, kwani ana uwezo mkubwa.” 
Alichosema Haruna Niyonzima kuhusiana na ishu ya Mavugo kuondoka Simba SC Alichosema Haruna Niyonzima kuhusiana na ishu ya Mavugo kuondoka Simba SC Reviewed by Zero Degree on 11/27/2017 04:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.