Loading...

TANESCO yaanza kubomoa jengo lake kutekeleza agizo la Rais Magufuli

Jengo la TANESCO Makao Makuu- Ubungo, Dar es salaam
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza hatua ya ubomoaji kwenye sehemu ya jengo lake kama utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alilotoa mwanzoni mwa mwezi huu ili kupisha ujenzi wa daraja la juu la ubungo.

Taarifa iliyotolewa na Tanesco kwa Vyombo vya Habari leo Novemba 27, 2017.

“Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unawafahamisha Wateja wake wote na Wananchi kwa ujumla kuwa TANESCO imeanza utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli, kuhusu kubomolewa kwa Jengo la Ofisi za TANESCO Makao Makuu, liliopo Ubungo Jijini Dar es salam. Kuanzia Jumatatu Novemba 27, 2017. Ukuta wa mbele ya jengo umesha vunjwa, pia baadhi ya Watumishi wa Shirika wameanza kuhamishiwa katika ofisi nyingine za TANESCO zilizopo jijini Dar es salaam ili kupisha shughuli za ubomoaji kufanyika kwa usalama zaidi. Uongozi wa Shirika pamoja na Wakala wa Majengo TBA wanaendelea kufanya taratibu zitakazo wezesha zoezi la ubomoaji wa Jengo kufanyika bila kuathiri huduma kwa Wateja wa Shirika. Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais. Tunapenda kuwahakikishia Wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa Huduma za Umeme zitaendelea kupatikana kama kawaida ikiwemo huduma ya manunuzi ya LUKU. Uongozi wa Shirika utaendelea kutoa taarifa kwa kadri zoezi hili linavyo endelea.”

Mapema mwezi huu Rais Dkt John Pombe Magufuli wakati akikagua ujenzi wa daraja la ghorofa tatu barabara ya Ubungo, aliamuru sehemu ya jengo la TANESCO na jengo la Idara ya maji kwenye eneo la barabara kuvunjwa ili kupisha ujenzi huo.
TANESCO yaanza kubomoa jengo lake kutekeleza agizo la Rais Magufuli TANESCO yaanza kubomoa jengo lake kutekeleza agizo la Rais Magufuli Reviewed by Zero Degree on 11/27/2017 05:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.